Mjane wake Justus Murunga ataka aruhusiwe kumzika mumewe

0

Mjane wake mbunge wa Matungu Justus Murunga amewasilisha kesi ya dharura mahakamani akitaka mahakama kubatilisha uamuzi wa kuzuia kumzika mumewe.

Christable Murunga kupitia kwa wakili wake Patrick Lutta anasema kesi iliyowasilishwa mahakamani na Agnes Wangui anayedai kuzaa watoto wawili na marehemu imeiletea familia hiyo mahangaiko makubwa.

Ameitaka mahakama kuruhusu kuendelea kwa mazishi yaliyokuwa yameratibiwa kufanyika tarehe Ishirini na saba na Ishirini na nane mwezi huu.

Mjane hiyo aidha anataka Wangui kulazimishwa kulipa Sh10M kama gharama ya kesi hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here