Mitaa inayokosa umeme zaidi Nairobi

0

Kwa mujibu wa ripoti ya wizara ya kawi, mitaa ya Nairobi West, Lang’ata, Karen, Lavington, Kibera na Rongai ilishuhudiwa kiwango cha chini cha kupotea kwa nguvu za umeme katika kipindi cha kati ya Julai 2016 na Julai mwaka huu.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, mitaa ambayo imeathirika sana na kupotea kwa nguvu za umeme ni Roysambu, Runda, Githunguri, Baba Dogo na Kiambu.

Kwa ujumla, taifa nzima limekuwa likikosa umeme kati ya saa mbili na saa nne kila mwezi.

Hata hivyo kwa wakaazi wa Highridge, Westlands na Kitisuru, wamekuwa wakikaa bila nguvu za umeme kwa kati ya saa tatu na saa sita kila mwezi.

Wakaazi wengine ambao wamekuwa wakikosa sana nguvu za umeme kwa kati ya nusu saa na saa mbili kila mwezi ni wale wa Embakasi, Dandora, Mombasa road, Umoja, Tassia na Ruai.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here