Ziara ya Rais Wiliiam Ruto inapotarajiwa kukamilika hii leo je na matunda zipi zilizovunwa na Kenya katika ziara hio ya siku tano?
Kenya imetia saini makubaliano kuhusu ujenzi wa barabara ya mwendokasi kutoka Mji wa Mombasa hadi Nairobi kwa kima cha shilingi. Bilioni mia nne sabini na saba itakayochukua miaka mitatu hadi mine kukamilishwa.
Aidha Marekani imetoa msaada wa helikopta 16 aina ya Hueys na MD 500 kwa vikosi vya ulinzi.
Wanafunzi 60 wa kenya aidha wanatajiwa kupata ufadhili wenye thamani ya ksh. 450 milioni kusomea marekani huku ufadhili wa milioni mia tisa ukitolewa na Washington DC kuboresha kikosi cha polisi na milioni mia mbili kwa magereza.
Fedha za marekani aidha zitatumia kwa ulinzi wa wafichuzi wa ufisadi, ulinzi wa jamii na maeneo mengine.
Kenya aidha imetambuliwa kama mshirika wa karibu wa marekani asiyekua mwanachama wa Muungano wa Usalama wa Atlantiki Kaskazini.