Michael Joseph ateuliwa mwenyekiti wa bodi ya Safaricom

0

Mwenyekiti wa bodi ya shirika la ndege nchini KQ Michael Joseph ameteuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa bodi ya kampuni ya mawasiliano ya Safaricom.

Katika taarifa, afisa mkuu mtendaji wa Safaricom Peter Ndegwa amesema Michael anachukua nafasi yake Nicholas Nganga ambaye amestaafu baada ya kuhudumu kwa miaka kumi na tatu.

Michael ataanza kazi Jumamosi hii tarehe mosi Agosti, siku ambayo shirika analoliongoza sasa la KQ linaanza safari zake za kimataifa ambazo zilisitishwa zaidi ya miezi mitatu iliyopita kutokana na janga la corona.

Hata hivyo Michael hatajiuzlu kama mwenyekiti wa bodi ya KQ na badala yake ataendelea kuhudumu katika afisi zote mbili.

Michael ndiye afisa mkuu mtendaji wa kwanza wa kampuni hiyo kubwa zaidi ya mawasiliano nchini na Ndegwa anasema ana tajriba ya kutosha kuleta mabadiliko yanayofaa.

Itakumbukwa kwamba ni chini ya uongozi wake ambapo Safricom ilizindua njia ya kutuma pesa kupitia kwa simu almaarufu M-pesa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here