Mfumo wa ugavi wa mapato: Yattani kufanya kikao na washikadau

0

Hazina ya kitaifa imeitisha kikao cha dharura hii leo kati ya baraza la magavana na uongozi wa bunge la seneti kuhusiana na mfumo wa ugavi wa mapato.

Waziri wa hazina ya Kitaifa Ukur Yattani anasema kikao hicho kinalenga kutafuta suluhu la mgogoro uliopo kwa sasa kuhusiana na mfumo ambao unafaa kutumika kugawa pesa baina ya serikali za kaunti.

Yattani anasema iwapo kikao cha bunge la seneti kesho kitakosa kuapata suluhu, serikali za kaunti zitashindwa kupata hela za kulipa mishahara na kuendesha shughuli zingine.

Kwa sasa kuna shilingi billion 316.5 ambazo serikali za kaunti zinafaa kugawana mwaka huu wa kifedha.

Jumla ya kaunti kumi na nane zitapoteza mabilion ya pesa iwapo mfumo unaopendekezwa wa kugawa pesa kutokan ana idadi ya watu utatumika.

Wiki iliyopita, maseneta kwa mara ya sita walikosa kuafikia suluhu katika vikao ambavyo vilifanyika hadi saa tatu usiku.

Hapo keho, maseneta watajadili mfumo unaopendekezwa na seneta wa Nairobi Johnson Sakaja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here