Mbunge wa zamani Makadara Benson Mutura, spika mpya wa Nairobi

0

Aliyekuwa mbunge wa Makadara Benson Mutura ndiye spika mpya wa bunge la kaunti ya Nairobi kufuatia kujiuzulu kwa mtangulizi wake Beatrice Elachi.

Mbunge huyo wa zamani ameibuka mshindi baada ya kuwashinda wagombea wenzake watano kwa kupata kura 99 kati ya 123.

Watu wengine waliokuwa wanawania wadhifa huo ni; Abdi Ali, Odingo Washington, Mike Guoro, Allan Mang’era pamoja Kennedy Ng’ondi.

Elachi alijiuzulu wiki hii kwa madai ya kuhofia maisha yake kutokana na malumbano ambayo yamekuwepo katika bunge hilo mara kwa mara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here