Mbunge wa zamani Kenn Nyagudi aaga dunia

0

Aliyekuwa Mbunge wa Kisumu Magharibi Kenn Nyagudi amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula amethibitisha kifo chake kwenye akaunti yake rasmi katika mtandao wa kijamii wa X.

Kulingana na spika Wetangula, mbunge huyo wa zamani alifariki siku ya Jumapili alipokuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta.

“Ninatuma rambirambi zangu kwa familia ya aliyekuwa Mbunge wa Kisumu Mjini Magharibi Kasisi Kenn Nyagudi. Nilipata fursa ya kutangamana naye nilipokuwa Waziri wa Masuala ya Kigeni,” amesema.

“Alifariki jioni ya leo alipokuwa akitibiwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta. Familia yake ipate faraja katika mikono ya Bwana,” ameongeza.

Mbunge huyo wa zamani alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2004 wakati wa uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha Joab Omino mnamo Januari mwaka huo huo.

Mbunge huyo alihudumu kwa miaka minne hadi alipopoteza kiti hicho wakati wa uchaguzi wa mwaka 2007 kwa Olago Aluoch.

Kifo cha Nyagudi kinajiri takriban mwezi mmoja baada ya aliyekuwa Mbunge wa Baringo Kaskazini Willy Rotich Kamuren kufariki alipokuwa akipokea matibabu Nairobi Ijumaa, Februari 28.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here