Mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua ahojiwa na DCI

0

Mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua amehojiwa katika makao makuu ya idara ya upelelezi nchini DCI kuhusiana na madai ya ufujaji wa Sh12.5b pesa za umma.

Gachagua anahojiwa siku moja baada ya kubainika kwamba akaunti zake za benki zimefungwa huku majasusi wakichunguza ni vipi kiasi kikubwa cha pesa kilipatikana kwenye akaunti zake.

Mbunge huyo anatuhumiwa kuwatumia washirika wake kupata kandarasi kwa kampuni Ishirini na mbili zinazohusishwa naye kwa kutumia njia la kilaghai.

Hata hivyo mbunge huyo amejitenga na madai ya ulaghai kwenye sakata hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here