Mbunge Sudi asema maisha yake hatarini

0

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi sasa anasema maisha yake yamo hatarini baada ya kunyanganywa walinzi wake wa kibinafsi.

Na sasa mbunge huyo aliyeshtakiwa kwa kutumia matamshi ya chuki anaitaka mahakama kutoa agizo linaloilazimisha idara ya Polisi kumrudishia walinzi wake anaosema alinyanganywa kinyume cha sheria.

Sudi amewasilisha kesi mbele ya hakimu mkaazi wa mahakama ya Nakuru K. L. Orege kupitia wakili wake Kipkoech Ng’etich.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here