Mbunge Oscar Sudi aachiliwa huru lakini afunge mdomo

0

Mahakama kuu imebatilisha uamuzi wa mahakama ya hakimu na kumuachiliwa kwa dhamana ya Sh500, 000 mbunge wa Kapseret Oscar Sudi aliyeshtakiwa kwa kutumia matamshi ya uchochezi.

Sudi kupitia kwa mawakili wake wakiongozwa na Nelson Havi walikata rufaa dhidi ya uamuzi wa hakimu Josephat Kalo kuruhusu Polisi kumzuilia kwa siku saba mbunge huyo ili kukamilisha uchunguzi dhidi yake.

Jaji wa mahakama kuu ya Nakuru Joel Ngugi ameamuru kuwa uamuzi wa kuendelea kumzuilia mbunge huyo ulikiuka katiba kwani upande wa mashtaka haukudhibitisha kwamba ana uwezo wa kuhitilafiana na mashahidi.

Hata hivyo jaji huyo amemzuilia mbunge huyo dhidi ya kuandaa mikutano yoyote ya hadhara au kutoa matamshi yoyote ya hadhara.

Jaji huo aidha amemuagiza Sudi kufika katika kituo chochocte cha Polisi atakapohitajika ili kusaidia katika uchunguzi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here