Mbunge Jonah Mburu akamatwa kwa ufisadi

0

Mbunge wa Lari Jonah Mburu Mwangi pamoja  na watu wengine watano wameshikwa na maafisa wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC kuhusiana na ufujaji wa Sh27M.

Mheshimiwa huyo na wenzake wanatazamiwa kulala seli wikendi hii baada ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Hajji kuidhinisha kushtakiwa kwao.

Mbunge na pamoja wenzake wakiwemo wanachama wa kamati inayosimamia pesa za ustawishaji maeneo bunge CDF wanatuhumiwa kupokea pesa kutoka kwa kampuni zilizofanya biashara na hazina hiyo ya CDF.

Mashtaka dhidi ya washukiwa hao ni pamoja na; kushirikiana kutekeleza ufisadi, matumizi mabaya ya afisi, kukosa kuzingatia sheria za ununuzi sawa na kuguza mali isiyo halali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here