Mbunge Johana Ng’eno kushtakiwa kwa uchochezi

0

Mbunge wa Emurua Dikkir Johanna Kipyegon Nge’no atashtakiwa kwa kutumia matamshi ya uchochezi wikendi iliyopita.

Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Hajji ameidhinisha kushtakiwa kwa mbunge huyo kwa misingi kwamba matamshi hayo yanalenga kusababisha uhasama miongoni mwa jamii zinazoishi Trans Mara kaunti ya Narok.

Hajji katika taarifa amesema ana ushahidi wa kutosha kudhibitisha kuwa matamshi hayo yaliyojumuisha matusi yana uwezo wa kuvuruga amani.

Wakati uo huo

Tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa (NCIC) imeelezea wasiwasi wake kuhusu hatua ya baadhi ya viongozi  kutoa matamshi yanayolenga kusababisha uadui miongoni mwa Wakenya.

NCIC katika taarifa badala yake inawashauri viongozi kuwa makini na matamshi yao ili kuepuka kuwagawanya Wakenya.

Onyo la tume hiyo linawadia huku matamshi ya wabunge Johanna Ng’eno wa Emurua Dikkir na mwenzake wa Kapseret Oscar Sudi kumhusu rais Uhuru Kenyatta kuibua hisia kinzani miongoni mwa Wakenya.

Wito sawia na huu umetolewa na naibu rais William Ruto ambaye amewakanya wendani wake dhidi ya kumtukana na kumdhalalisha rais Uhuru Kenyatta licha ya kutofautiana naye.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here