Mbunge Didmus Barasa kufungwa jela iwapo hatalipa deni

0

Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa ana hadi Jumanne kumlipa wakili Alfred Ndambiri deni lake la Sh1.8M au asukumwe jela miezi sita.

Barasa anadaiwa kukataa kumlipa wakili huyo pesa zake baada ya kumwakilisha kesi ya kupinga uchaguzi wake mwaka 2017 kwenye kesi iliyowasilishwa mahakamani na aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Suleiman Murunga.

Wawili hao wamekuwa wakidaiana deni hilo kuanzia wakati huo ndiposa wakili huyo akaamua kumushtaki mbunge huyo mbele ya hakimu D.M Kivuti.

Barasa amefika mbele ya hakimu huyo mara saba akiahidi kulipa deni hilo lakini hajatekeleza ahadi hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here