Mbunge Didmus Barasa ashtakiwa kwa ulaghai

0

Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa Wekesa ameachiliwa kwa shilingi laki moja pesa taslimu baada ya kukanusha madai ya kuuza gari kwa kutumia njia za kilaghai kwa mfanyibiashara mmoja huko Kitengelea.

Mbunge huyo amefikishwa katika mahakama ya Kajiado ambapo ameshtakiwa kwa madai ya kutumia uongo kupokea Sh450, 000 kutoka kwa mfanyibiashara John Irungu Mwangi mwaka 2017 akimhadaa kwamba angemuuzia gari.

Barasa anayewakilishwa na wakili John Khaminwa ameshtakiwa baada ya jaribio lake kuwasilisha kesi mahakamani kuzuia kukamatwa na kufikishwa mahakamani kuambulia patupu.

Alidai kwamba masaibu yanayomuandama yanahusishwa na yeye kumuunga mkono naibu rais William Ruto katika azma yake kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2022.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here