Mauji ya Omwenga: Obure na Ouko kusalia kizimbani zaidi

0

Washukiwa wakuu kwenye mauaji ya Kevin Omwenga katika eneo la Kilimani, Nairobi Chris Obure na Robert Ouko wataendelea kulala kizimbani kwa siku saba zaidi wakisubiri uamuzi wa mahakama kuhusu ombi lao la kuachiliwa kwa dhamana.

Wawili hao wamefikishwa mbele ya jaji Jessie Lessit Jumatatu ambaye ameagiza wazuiliwe kwa siku saba zaidi wakisubiri hatma yao.

Upande wa mashtaka unapinga ombi la washukiwa hao kuachiliwa kwa dhamana kwa misingi kwamba watahitilafiana na ushahidi iwapo wataachiliwa huru.

Aidha upande wa mashtaka umeifahamisha mahakama kwamba huenda Obure na Ouko watakwepa kuhudhuria vikao vya mahakama iwapo ombi lao la dhamana litaridhiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here