Matiang’i awaonya Polisi dhidi ya kutumiwa na wanasiasa

0

Waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i amewaonya maafisa wa Polisi dhidi ya kutumiwa vibaya na wanasiasa  wakati wa mchakato unaoendelea wa kubadilisha katiba kupitia BBI.

Dkt. Matiang’i amesema ni jukumu la Polisi kuwapa usalama viongozi wote wanapoendelea na mjadala huo pasipo kuegemea upande wowote.

Waziri Matiangi amesema haya alipofunga rasmi warsha ya siku mbili ya kutoa mafunzo kwa makamanda wa Polisi wa maeneo mbalimbali katika jumba la mikutano la KICC.

Wakati hayo yakijiri

Muungano wa mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yanayoshinikiza mabadiliko katika idara ya Polisi yametofautiana na mapendekezo yanayotolewa kwenye ripoti ya BBI kubadilisha sura ya idara ya Polisi.

Mashirika hayo yanayojumuisha Amnesty International, Transparency International (TI) na IMLU chini ya uongozi wake mkurugenzi mkuu Peter Kiama yanahoji kuwa kubuniwa kwa baraza kuu kusimamia idara ya Polisi itaruhusu kuingiliwa kwa idara ya hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here