Matiangi akutana na wanamitumba

0

Waziri wa usalama wa ndani  Dr Fred Matiangi amekutana na muungano wa wafanyibiashara wa mitumba kujadili mikakati  ya kuwezesha uagizaji bidhaa hizo nchhini.

Kikao cha leo kimelenga kujadili mwongozo ambao utatumika kuagiza mitumba nchini kufuatia agizo la Rais Uhuru Kenyatta.

Kwenye hotuba yake kwa taifa Rais alisema marufuku iliyowekwa kuagiza mitumba nchini kutokana na hofu ya kusambaa kwa virusi vya corona imeondolewa.

Wafanyibishara hao wamekuwa wakishinikiza kuruhusiwa kuagiza bidhaa hizo nchini na kusema kuwa walikuwa wamekosa bidhaa za kuuza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here