Mataifa 7 zaidi yaruhusiwa kuingia Kenya

0

Mataifa 7 zaidi yameongezwa kwenye orodha ambayo raia wake wataruhusiwa kuingia nchini kuanzia kesho wakati Kenya itarejelea safari zake za kimataifa.

Mataifa hayo ni pamoja na Marekani (lakini sio California, Florida na Texas), Uingereza, Ufaransa, Uholanzi, Qatar, Italia na mataifa yaliyoko Milki za Kiarabu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka wizara ya uchukuzi, mataifa hayo saba yanajiunga na China, Korea Kusini, Japan, Canada, Zimbabwe Ethiopia, Switzerland, Rwanda, Uganda, Namibia na Morocco ambayo tayari raia wake watapata kibali cha kuingia nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here