Matabibu watoa makataa ya siku saba kugoma

0

Matatibu wametoa ilani ya siku saba kugoma kulalamikia kile wanataja kama kubaguliwa na kutopandishwa vyeo.

Mwenyekiti wa muungano wa matabibu (KUCO) Peter Wachira amesema kuwa masuala ambayo shirika linalosimamia huduma za Nairobi (NMS) imekosa kutimiza ni kulipwa mishahara yao kwa wakati na kupandishwa kwa vyeo kwa madaktari waliofanya kazi kwa muda mrefu.

Mgomo huo unatazamiwa kuanza tarehe 29 mwezi huu wa Octoba.

Hayo yakjiri, wauguzi katika kaunti ya Nakuru wamehofia afya yao haswaa wakati huu wa corona ambapo wanasema mazingira mabaya ya kufanyia kazi yamesababisha baadhi yao kuambukizwa virusi hivyo.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here