Mashirika ya binadamu yaishtaki serikali

0

Mashrika mbalimbali ya kutetea haki za kibinadamu yameishtaki serikali kutokana na madai ya maafisa wa polisi kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa kutekeleza masharti ya kuzuia msambao wa virusi vya corona.

Katika kesi hiyo, mashrika hayo yakiwemo Amnesty International, Haki Afrika, na kituo cha Sheria wanataka mahakama ishurutishe serikali kuwalipa walio dhulmiwa na maafisa wa polisi na pia familia za waliopoteza maisha yao.

Wanataka mahakama kuamuru pia kuwa polisi walikiuka sheria za kulinda haki za kibinadamu wakati wakitekeleza masharti hayo ikiwemo agizo la kutotoka nje.

Mashirika hayo yanasema tangu siku ya kwanza serikali ilitoa mari ya kutotoka nje, polisi wamekuwa wakiwadhulumu watu wanaokiuka amri hiyo hatua ambayo wanasema ni kinyume na haki za kibinadamu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here