Masharti makali katika maabadi yarejeshwa

0

Baraza lililobuniwa kuangazia kufunguliwa kwa sehemu za kuabudu limetengaza kurejelewa kwa masharti makali kuzuia msambao wa virusi vya corona kufuatia kuongzeka kwa idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini.

Naibu mwenyekiti wa baraza hilo Dkt. Connie Kivuti ametangaza kuwa ibada zitadumu kwa muda wa dakika tisini huku waumini watakaoruhusiwa kuhudhuria ibada wakiwa ni wale walio na umri wa miaka sita hadi sitini na tano.

Baraza hilo ambalo limewasuta wanasiasa kwa kutumia visivyo maabadi vile limetangaza kuwa watakaohudhuria mazishi watakuwa ni watu mia moja pekee, harusi itahudhuriwa na watu hamsini huku chakula kikipigwa marufuku kwenye sherehe hizo.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here