Maseneta wapinga KMC kupewa KDF

0

Maseneta wamekosoa hatua ya serikali kuhamisha usimamizi wa tume ya nyama (KMC) hadi katika wizara ya ulinzi.

Maseneta wakiongozwa na Steward Madzayo wa Kilifi wametaja hatua hiyo kama ukiukaji wa sheria kwani tume hiyo inafaa kuwa chini ya wizara ya mifugo.

Seneta wa Machakos Boniface Kabaka ndiye aliwasilisha hoja ya kutaka maelezo kutoka kwa serikali kuhusu ni kwa nini KMC ilihamishwa hadi katika wizara ya ulinzi.

Waziri wa Kilimo Peter Munya ametetea hatua hiyo ya rais Uhuru Kenyatta akisema mteja mkubwa wa KMC ni wizara ya ulinzi na hivyo kuipa usimamizi wake kutaiwezesha tume hiyo kuboreshwa zaidi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here