Bunge la seneti kwa mara nyigine limeahirisha vikao vya kujadili mswada tata wa ugavi wa mapato hadi Jumanne wiki ijayo.
Spika Ken Lusaka anasema wamepokea ripoti ya kamati maalum iliyobuniwa kutafuta suluhu na kikao kisicho rasmi almaarufu Kamkunji kitaandaliwa Jumatatu ijayo kujaribu kuafikia mwafaka wa pamoja.