Maseneta wahairisha mswada wa ugavi wa mapato tena

0

Bunge la Senate kwa mara ya saba wamehairisha mjadala wenye utata kuhusu ugavi wa mapato katika serikali za kaunti.

Maseneta 34 walipiga kura kuunga mkono hoja hiyo yake seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen huku 26 wakipinga.

Akiwasilisha hoja hiyo, Murkomen ambaye alikuwa kiongozi wa walio wengi katika bunge hilo alihoji kwamba kuhairishwa kwa mjadala huo kutatoa nafasi kwa mashauriano zaidi na kuliepusha taifa dhidi ya kugawanyika zaidi.

 Mjadala huo umesababisha migawanyiko nchini baadhi ya viongozi wakilalamikia kubaguliwa katika mfumo wa ugavi wa pesa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here