Jaji mkuu anayeondoka David Maraga amesisitizia umuhimu wa idara ya mahakama kusalia huru kwenye hotuba yake ya mwisho.
Maraga ametaja kupunguzwa kwa mrundiko wa kesi mahakamani kama hatua kubwa aliyoingoza idara hiyo kupiga wakati wa uongozi wake ila akataja kuwa kukosa kuwateua majaji arobaini na moja alivyofanya rais Uhuru Kenyatta haikufaa.
Rais huyo wa mahakama ya upeo vile vile amelalamikia kupunguzwa kwa bajeti ya idara ya mahakama tangu ilipofutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais mwaka 2017 hatua ambayo imelemaza shughuli nyingi ikiwemo kujengwa kwa mahakama katika sehemu mbalimbali nchini.
Maraga anayestaafu mapema mwaka ujao amesema anajivunia alichofanya wakati wa hatamu yake akisema licha ya kutofautiana na rais Kenyatta, hana kinyongo naye.