Maraga alaumiwa kwa kuhujumu mchakato wa kumsaka mrithi wake

0

Jaji mkuu David Maraga ameshutumiwa kwa kuhujumu juhudi za kumtafuta mrithi wake kama rais wa mahakama ya upeo.

Macharia Njeru, mwakilishi wa chama cha Mawakili nchini (LSK) katika tume ya huduma za mahakama (JSC) anamtuhumu Maraga kwa kuvuruga mchakato huo kwa kuwatumia wendani wake katika idara ya mahakama.

Njeru anadai kuwa Maraga anamtumia naibu wake Phlomena Mwilu na jaji Mohamed Warsame kuzuia kuanza mchakato huo wa kumrithi.

Maraga anatazamiwa kuelekea kwenye likizo Disemba 15 kabla ya kustaafu kwake Januari 21 mwaka ujao 2021.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here