Jaji mkuu David Maraga hatimaye amebuni jopo la majaji watano kuskiliza kesi ya kupinga bunge kuvunjwa alivyomshauri Rais Uhuru Kenyatta
Jopo hilo linaongozwa na jaji Lydia Achode na majaji wengine ni George Odunga, James Makau, Anthony Ndungu na Pauline Nyamweya.
Mahakama kuu ilimtaka Maraga kubuni jopo kuskiliza kesi iliyowasilishwa na wakenya wawili wanaopinga bunge kuvunjwa kwa msingi kuwa suala hilo linaibua masuala yenye uzito kikatiba.
Tume ya huduma za bunge PSC pia ilielekea mahakamni kupinga ushauri huo wa Maraga baada ya wabunge kushindwa kupitisha mswada wa usawa wa jinsia kwa mujibu wa katiba ya 2010.