Rais Uhuru Kenyatta amepigia debe BBI jijini Nairobi akiwasihi wakenya kuisoma na kuiunga mkono ili kuleta umoja katika taifa hili.
Akizungumza katika eneo la Pumwani alipokuwa ameenda kukutana na viongozi wa bodaboda rais amewataka wakenya kusoma ripoti ya BBI na kuelewa kisha kuiunga mkono ili kuwa na taifa lenye amani na umoja.
Hayo yakijiri
Nalo Baraza la magavana kupitia gavana wa Tharaka Nithi Muthomi Njuki limeunga mkono ripoti hiyo ya BBI likisema kwamba itasaidia pakubwa katika kuimarisha sekta ya Kilimo.
Naye gavana wa Kitui Charity Ngilu amesema mapendekezo ya BBI iwapo yatatekelezwa yatawezesha kuletwa kwa rasilimali zaidi katika serikali za kaunti.
Kwingineko
Mwakilishi wa akina mama katika kaunti ya Murang’a Sabina Chege ametaka mjadala zaidi kuhusu pendekezo la kuondolewa kwa wadhifa wa mwakilishi wa wanawake kwenye ripoti ya BBI.
Ametofautiana na wazo hilo akisema hatua hiyo itakuwa ni kuwapokonya wanawake nafasi walizotengewa kikatiba.
Rais Kenyatta anatarajiwa kuzindua rasmi ripoti ya BBI siku ya Jumatatu kwenye ukumbi wa Bomas.