Bodi ya shirika la kusambaza dawa na vifaa vingine vya matibabu nchini KEMSA sasa inamtuhumu afisa mkuu mtendaji aliyesimamishwa kazi Dr Jonah Manjari kwa kwa kufanya maamuzi bila kuwahusisha.
Mwenyekiti wa bodi hiyo Kembi Gitura anasema Dr Manjari aliiandikia hazina ya kitaifa na kuomba kuwapa shilingi billion 7.1 ilehali bodi hiyo ilikuwa imeidhinisha KEMSA kupewa shilingi billion 4.6 pekee.
Manjari ambaye amebadili msimamo wake kuwa alishinikizwa kutoa zabuni kwa baadhi ya kampuni amesema kuwa hakuna pesa zozote zilipotea chini ya usimamizi wake.
Akifika mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu Afya chini ya uenyekiti wake mbunge wa Murang’a Sabina Chege, katibu katika wizara ya uchukuzi Christopher Obure amesema baadhi ya vifaa havikufika nchini kutoka Ethopia kuashiria kuwa huenda vilipotea kwa ndege au nchini Ethiopia.