Mama na mwanawe wafariki baada ya kupigwa na stima Ukunda

0

Mama na mwanawe wamefariki ghafla baada ya kupigwa na stima katika eneo la Ukunda kaunti ya Mombasa Ijumaa 31-07-2020.

Mama huyo aliyekuwa amembeba mwanawe mgongoni alikanyaga nyaya hizo za stima pasipo kujua alipokuwa anarejea nyumbani.

Wenyeji wanasema juhudi za mara kwa mara kujaribu kufahamisha kampuni ya Kenya Power kuhusu hatari ya nyaya hizo zimeambulia patupu hatua zozote zisichukuliwe.

Hata hivyo Kenya Power katika taarifa inasema inasikitikia tukio hilo na kusema imeanzisha uchunguzi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here