Mama amuuza mtoto shilingi elfu moja

0

Maafisa wa polisi katika kaunti ya Machakos wanamzuilia mama mmoja ambaye anadaiwa kuuza mtoto wake kwa shilingi elfu moja.

Winnierose Mumbe kutoka kaunti ya Kitui anatuhumiwa kumuuzia mtoto wake Tina Mulinge miezi mitatu iliyopita.

Tina anadaiwa kupotea nyumbani kw amuda wa miezi tisa, na aliporejelea akasema kuwa alikuwa amepata mtoto kimiujiza, licha ya kuwa hana uwezo wa kupata watoto.

Wachunguzi pia wanasema kuna mama mwingine ambaye amejitokeza akidai kuwa mtoto mwingine wa Tina Mulinge, mwenye umri wa miaka mitano ni wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here