Makabila manne makuu nchini, Kikuyu, Kalenjin, Luhya na Luo yanaendelea kuwa na wafanyikazi wengi serikalini kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa wizara ya huduma za umma.
Ripoti hiyo iliyowasilishwa bungeni na waziri Margret Kobia inaonyesha kuwa kati ya maafisa wakuu 417 serikalini, 120 kati yao wanatoka katika jamii ya Kikuyu, huku jamii za Wakalenjin, Wajaluo, Waluhya na Wakamba zikiwa na wafanyikazi 45, 41, 33 na 27 mtawalia.
Na katika mashirika takribani 286 ya kiserikali, wengi wa wakurugenzi wanatoka katika jamii za Kikuyu na ile Kalenjin ambazo ziko na wakurugenzi 36 na 35 mtawalia.









