Mahakama ya Leba imesitisha uteuzi wa Pauline Njoroge na watu wengine wanne kuhudumu kwenye bodi ya Utalii nchini.
Jaji Hellen Wasilwa amesitisha uteuzi huo uliofanywa na waziri wa Utalii Najib Balala kufuatia kesi iliyowasilishwa mahakamani na chama cha mawakili nchini LSK.
LSK kwenye kesi yake inashangaa ni vipi Pauline Njoroge aliteuliwa kwenye bodi hiyo na kisha baadaye waziri Balala akaubatilisha na kumteua Najma Ismael.
Na iwapo uteuzi huo utasalia, LSK inahoji kuwa bodi hiyo itakuwa na watu ambao hawafai kuhudumu kwani wamechaguliwa tu pasipo kuwa na shughuli ya kuwapiga msasa ipasavyo.