Mahakama kuu imesitisha utekelezwaji wa agizo la rais Uhuru Kenyatta linaloziweka asasi zote huru chini ya afisi ya mwanasheria mkuu na mawaziri.
Akitoa uamuzi huo, jaji John Mativo ameamuru kwamba rais alitumia mamlaka yake visivyo kutoa agizo hilo kufanya mabadiliko kwenye asasi hizo muhimu zinazopaswa kuwa huru kikatiba.
Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na chama cha mawakili nchini (LSK).
Agizo hilo lililotolewa na rais Uhuru Kenyatta May 11, 2020 lingeathiri tume zipatazo 20 ikiwemo tume ya huduma za umma, tume ya huduma za bunge, tume ya maadili na kupambana na ufisadi (EACC), tume ya huduma za mahakama (JSC), tume ya huduma za walimu (TSC) miongoni mwa zingine.









