MAHAKAMA YARUHUSU MIILI 120 ILIYOHIFADHIWA KATIKA MAKAFANI YA NAIROBI KUTUPWA

0
nairobi funeral home
nairobi funeral home

Mahakama kuu imekataa kutoa agizo la kuzuia serikali ya kaunti ya Nairobi kutupa maiti 120 ambazo hazijachukuliwa na familia katika makafani ya Nairobi ; hatua ambayo sasa inapisha njia kwa kaunti ya Nairobi kutupa miili hio.

Jaji Lawrence Mugambi amesema sababu zilizotolewa na Chama cha Wanasheria nchini Kenya (LSK) kutaka kusimamisha notisi iliyotolewa na kaunti ya kutupa miili hiyo haina mshiko.

LSK katika kupinga uamuzi wa kaunti ilisema vijana wengi waliofariki kufuatia maandamano ya kupinga mswada wa fedha wa 2014 walipelekwa katika chumba hicho cha kuhifadhi maiti.

“Familia nyingi katika Jiji la Nairobi na kwingineko humu nchini zimekuwa zikiwatafuta wapendwa wao ambao wametoweka tangu maandamano hayo kuanza,” ilisema LSK.

Lakini Mugambi kwa kukataa kutoa agizo hilo amesema:

“Agizo lililoombwa na LSK sio mahususi na si halali kwani wananchi kwa ujumla wanapewa fursa ya kutembelea chumba cha kuhifadhia maiti na kutambua miili hiyo kabla ya uamuzi wa kutupa miili kuafikiwa,” amesema.

Jaji Mugambi ameunga mkono hatua ya kaunti akisema lengo la notisi hiyo ni kufahamisha umma ili walio na kesi za watu waliopotea waende katika chumba cha kuhifadhi maiti kwa madhumuni ya kuwatambua.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here