Wabunge wana kila sababu ya kutabasamu baada ya mahakama kusitisha kwa muda utekelezwaji wa ushauri wa kulivunja bunge uliotolewa kwa rais Uhuru Kenyatta na jaji mkuu David Maraga.
Uamuzi huu umetolewa na jaji wa mahakama ya kikatiba Weldon Korir kufuatia kesi iliyowasilishwa mahakamani na walalamishi wawili Leina Konchella na Mohsen Abdul Munasar.
Jaji Korir ameamuru kuwa kesi hiyo inaibua maswala yenye uzito wa kikatiba na hivyo inafaa kuwasilishwa kwa jaji mkuu kubuni jopo la majaji kuisikiliza na kutoa uamuzi.
Chama cha Mawakili nchini LSK kimejumuishwa kwenye kesi hiyo inayotarajiwa kutajwa Octoba 7.