Mahakama ya Milimani, Nairobi itafungwa kwa siku 14 kuanzia Alhamisi tarehe 30, Julai baada ya mfanyikazi mmoja wa mahakama kupatikana na virusi vya corona.
Wakati wa kipindi hicho, jaji mkuu David Maraga amesema wafanyikazi wa mahakama hiyo watajiweka kwenye karantini huku juhudi za kuwatafuta waliotengamana na mgonjwa huo zikiendelea.
Ni maswala yenye umuhimu mkubwa na dharura ndiyo yatashughulikiwa ila kupitia kwa njia ya kimtandao kwa mujibu wa Maraga wakati mahakama hiyo itakuwa imefungwa.