Jaji wa mahakama kuu John Onyiengo amefutilia mbali hukumu ya miaka mitatu iliyokuwa imepewa aliyekuwa katibu mkuu Sammy Kirui kwenye sakata ya makaburi iliyogharimu Sh283M.
Onyiengo amemuachilia huru Kirui kwa misingi kwamba upande wa mashtaka ulikosa kutoa ushahidi wa kutosha kudhibitisha kwamba alitumia visivyo mamlaka yake.
Hata hivyo mahakama hiyo imeshikilia uamuzi wa kuwafunga jela miaka mitatu aliyekuwa mkurugenzi wa maswala ya kisheria katika lililokuwa baraza la jiji la Nairobi Mary Ngethe na aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya utoaji zabuni Alexandar Musee.
Uamuzi wa kuwahukumu washukiwa hao ulitolewa na hakimu Douglas Ogito mwaka 2018.