Magoha: Usalama wa wanafunzi kuzingatia kabla ya shule kufunguliwa

0

Waziri wa elimu Profesa George Magoha amesisitiza kwamba usalama wa wanafunzi utapewa kipau mbele kabla ya kufunguliwa tena kwa taasisi za masomo.

Akizungumza baada ya kukagua mikakati ya usalama inayowekwa na taasisi ya kutoa mafunzo ya kiufundi ya Siaya Jumatano, waziri Magoha amesema afya ya wanafunzi kuambatana na hali ya virusi vya corona nchini itaendelea kufuatiliwa ya kuidhinisha kufunguliwa kwa taasisi hizo.

Kabla ya kufanya ukaguzi huo, Profesa Magoha alifanya mashauriano na gavana wa kaunti hiyo ya Siaya Cornel Rasanga mapema asubuhi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here