Baraza la magavana limemtahadharisha rais Uhuru Kenyatta dhidi ya kulivunja bunge alivyoshauriwa na jaji mkuu David Maraga.
Mwenyekiti wa baraza hilo Wycliffe Oparanya amesema licha ya kwamba wanaelewa sababu za Maraga kumshauri rais kulivunja bunge, kutakuwa na athari kubwa katika uongozi wa taifa hili haswaa wakati huu ambapo tunapambana na janga la corona.
Badala yake baraza hilo linashauri kuwepo na mashauriano ya kina baina ya wadau wote ili kuafikia suluhu la kudumu kuhusu namna ya kuafikia usawa wa jinsia.