Magavana wanataka waruhusiwe kubaki ofisini hata wakishtakiwa kwa wizi

0

Mahakama kuu imeelekeza kesi ambapo baraza la magavana linataka magavana walioshtakiwa kwa ufisadi kuruhusiwa kuingia afisini kusikilizwa na jopo la majaji watatu.

 Jaji James Makau ametaja kesi hiyo kama ya dharura na kuratibu itajwe Octoba 21 mbele ya jopo hilo la majaji.

Baraza la magavana linahoji kuwa magavana wanaoandamwa na kesi za ufisadi wanazuiliwa kuingia afisini mwao na baadhi yao kuishia kubanduliwa mamlakani pasipo kufuatwa kwa utaratibu wa kisheria.

Magavana walioshtakiwa kwa ufisadi na kuzuiliwa kuingia afisini ni pamoja na Mike Sonko (Nairobi), Okoth Obado (Migori), Moses Lenolkulal (Samburu), Ali Korane (Garissa) na Muthomi Njuki (Tharaka Nithi).

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here