Madaktari nchini wametishia kugoma iwapo matatizo yanayokumba sekta ya afya hayatasuluhishwa.
Muungano wa madaktari nchini (KMPDU) kupitia kaimu katibu mkuu Dkt. Chibanzi Mwachonda unasema wahudumu wa afya wameendelea kutaabika ilhali serikali imekosa kuyapa kipau mbele maslahi yao.
Muungano huo unasisitiza kwamba changamoto katika sekta ya afya zitatatuliwa kupitia kubuniwa kwa tume ya huduma za afya sawa na inavyopendekezwa kwenye ripoti ya BBI.
Miongoni mwa changamoto wanazosema wanapitia ni pamoja na kulipwa mishahara duni pasipo kuzingatia kazi wanayofanya na kutotekelezwa kwa mikataba ya maelewano.