Madaktari wasisitiza kuwa mgomo wao bado upo

0

Madaktari wanasisitiza kwamba watagoma kuanzia tarehe sita mwezi ujao iwapo malalamishi yao hayatashughulikiwa.

Muungano wa madaktari nchini KMPDU kwenya taarifa iliyotumwa na kaimu katibu mkuu Chibanzi Mwachonda unasema licha ya kufanya mazungumzo na asasi husika za serikali, mazungumzo hayo yamekosa kuzaa matunda kufikia sasa.

Miongoni mwa masharti yao ni kwamba madaktari wote wapewa bima ya matibabu NHIF, kuajiriwa kwa madaktari 2,000 ambao hawana kazi, kulipwa kwa marupurupu yao yote na kupewa marupurupu ya kuhatarisha maisha yao wanapokuwa kazini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here