MADAKTARI WA KUTRRH WATISHIA KUGOMA KUANZIA KESHO

0

Madaktari kwenye hospitali ya Mafunzo ya Chuo Kikuu cha Kenyatta KUTRRH wametoa onyo ya masaa 24 ya kuenda kwenye mgomo.

Wakiiongozwa na Katibu Mkuu wa Muungano wa Madaktari KMPDU tawi la KUTRRH Dkt. Vincent Oyiengo madaktari hao wamelalamimikia hatua ya mwenyekiti wa Bodi ya hospiali Olive Mugendahio kuingilia utendakazi wa kila wa taassisi hio.

Madaktari hao hususan wamelalamikia hatua ya kupelekewa kwa likizo ya lazma afisa mkuu mtendaji Ahmed Dagane wakitaka bodi inayoongozwa na Mugenda kubanduliwa.

“Aliyeteuliwa na Profesa Mugenda na wapambe wake kuchukua nafasi ya Afisa Mkuu Mtendaji haja hitimu hata kuongoza Mochwari ya Hospitali hii” Amesema Dkt. Oyiengo.

Dagane wiki jana aliagizwa Kwenda kwenye likizo na nafasi yake kuchukuliwa na Issac kamau.

Uamuzi wa Kuteuliwa Kwa Kamau hata hivyo ilisitishwa na Wizara ya Afya ambayo iliagiza Dagane aaendelee kuhudumu hadi muhula wake utakapokamilika mwezi Machi Mwaka ujao.

Wafanyikazi hao aidha wanataka kurejeshewa bima yao ya afya na wenzao ambao wamelazimika kutumia fedha zao kupata matibabu kurejeshewa fedha hizo.

“Mugenda ametuondolea bima yetu. Ni sharti bimah io irejeshwe mara moja.” Ameongeza Dkt. Oyiengo.

Manesi wa hospitali hio wameunga mkono madaktari wakitishia sawia kuenda kwenye mgomo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here