Madaktari wawili wa Cuba waliotekwa nyara na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab mjini Mandera mwaka 2019 hatimaye wameachiliwa huru.
Wawili hao Landy Rodrigues na Herera Correa walitekwa wakati wanamgambo hao walishambulia gari lao na kuishia kumuua afisia mmoja wa Polisi aliyekuwa anawalinda.
Mamlaka nchini Somalia imedhibitisha kuwa madaktari hao wameachiliwa baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo.