Madaktari Nairobi watishia kugoma

0

Madaktari wa kaunti ya Nairobi wametoa makataa ya siku saba kugoma iwapo lalama zao hazitashughulikiwa.

Kupitia kwa katibu mkuu wa muungano wa madaktari KMPDU tawi la Nairobi Thuranira Kaugiria, madaktari hao wamelalamikia mazingira mabaya ya kufanyia kazi wakati huu taifa linapambama na janga la corona.

Kuu kwenye lalama zao ni kucheleweshwa kwa mishahara yao na kutokuwepo kwa vituo maalum vya kujitenga iwapo watapata corona wanapowahudumia wagonjwa.

Wametishia kuanza mgomo wao Agosti 21 iwapo serikali ya kaunti ya Nairobi itapuuza lalama zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here