Madaktari Nairobi wasisitiza mgomo wao ungalipo

0

Mgomo wa madaktari kaunti ya Nairobi utaendelea kama ilivyopangwa Ijumaa hii baada ya lalama zao kukosa kushughulikiwa.

Katibu mkuu wa muungano wa madaktari KMPDU tawi la Nairobi Thuranira Kaugiria amekiarifu kituo hiki kwa njia ya simu kwamba serikali inatumia vitisho dhidi yao badala ya kuwaita katika meza ya mazungumzo kutanzua mgomo huo.

Kuu kwenye lalama zao ni kucheleweshwa kwa mishahara yao na kutokuwepo kwa vituo maalum vya kujitenga iwapo watapata corona wanapowahudumia wagonjwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here