MACHIFU WATANO WATEKWA NYARA ENEO LA EL- WAK

0

Machifu watano wametoweka katika kisa kinachoshukiwa kuwa cha utekaji nyara kilichotekelezwa na wanamgambo wa Alshabaab eneo la Elwak, Kaunti ya Mandera.

Polisi na mashahidi wamesema kundi hilo la machifu lilikuwa likisafiri kwa gari kuelekea Elwak asubuhi ya leo walipovamiwa na kutekwa nyara kati ya Bamba Owla na Ires Suki.

Machifu hao walikuwa wakutane katika eneo hilo kupanga jinsi ya kudumisha usalama wakati wa ziara ya Rais William Ruto katika eneo hilo.

Kamanda wa polisi wa Mandera Kusini Julius Njeru amethibitisha kisa hicho akisema kuwa vikosi vya Jeshi la Kenya KDF vimeanzisha oparesheni kali ya kuhakikisha kuwa machifu hao wameachiliwa.

Rais William Ruto anatarajiwa kuandamana na wandani wake wakuu ikiwa ni pamoja na naibu wake Kithure Kindiki katika ziara hiyo.

Rais atatembelea kaunti za Mandera, Garissa na Wajir.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here