Maaskofu wa kanisa katoliki wakosoa BBI

0

Maaskofu wa kanisa katoliki wametoa wito kwa rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa chama wa cha ODM Raila Odinga kuruhusu kutathminiwa upya kwa ripoti ya BBI ili kujumuisha maoni ya wanaohisi kusahaulika.

Katika taarifa, maaskofu hao wametoa mtazamo wao kwa mapendekezo mbalimbali yanayotolewa kwenye ripoti hiyo.

Maaskofu hao wametofautiana na wazo la kumpa rais mamlaka ya kumteua waziri mkuu wakisema hilo halitatatua changamoto ya mshindi kuchukua kila kitu baada ya uchaguzi.

Viongozi hao wa kidini kadhalika wamepinga pendekezo la kuongeza idadi ya maseneta na kufikia tisini na nne, kuwaruhusu wanasiasa kuwateua makamishna wa tume ya uchaguzi IEBC na kuingilia uhuru wa idara ya mahakama.

Haya yanajiri siku moja baada ya viongozi wa kidini kutoka muungano wa kievanjilisti kuteta kuwa maoni yao yalipuuzwa kwenye ripoti hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here