Maambukizi ya corona nchini yapita 22, 000

0

Idadi ya watu waliofariki kutokana na virusi vya corona baada ya kisa cha kwanza kuripotiwa nchini imeongezeka na kufikia watu 369 baada ya watu watano zaidi kufariki.

Katika taarifa, wizara ya afya inasema kwa muda was aa ishirini na nne zilizopita, watu 690 wamepatikana na virusi hivyo na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 22, 053 kutoka kwa sampuli 315, 723 zilizochunguzwa tangu kisa cha kwanza kuripotiwa nchini.

 Kati ya visa hivyo 690, Niarobi inaendelea kuongoza kwa kurekodi visa 535, Kiambu 56, Kajiado 28, Nyeri24, Busia9 , Machakos 7, Nakuru 6, Kisumu 6, Embu 4, Garissa 4, Laikipia 3, Narok3.

Meru, Mombasa, Nyandarua, Bungoma na Kwale zina kesi moja.

 Kati ya visa hivyo 535 jijini Nairobi, Westlands 63, Langata 44, Dagoretti kaskazini na Dagorreti Kusini 43 kila moja, Embakasi mashariki 40, Starehe 38, Kamukunji 32, Makadara 30, Embakasi kusini 29, Kasarani 27, Kibra 25, Embakasi Magharibi 23 Roysambu 21, Embakasi kaskazini 20, Embakasi ya kati, Ruaraka na Mathare visa 19 kila moja.

Habari njema ni kuwa idadi ya waliopona baada ya kuambukizwa virsui hivyo imefikia 8,477 baada ya watu wnegine 58 kuondnoka leo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here